Na Mwandishi Wetu, Tanga.
NAIBU Waziri wa Nishati Judith Kapinga amegawa mituni ya gasi 1500 kwa wakazi wa Kijiji cha Msomela Handeni Wilayani Handeni mkoani Tanga iliyotolewa na Kampuni ya Taifa Gas.

Kutolewa kwa mitungi hiyo kwa wakazi hayo inalenga kuunga mkono kampeni ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk, Samia Suluhu Hassani ya kumtua mzigo wa kuni Mama kwa kutumia nishati ya Taifa Gas na kuhifadhi Mazingira.
Akishukuru msaada huo Naibu Waziri wa Nishati Kapinga amesema Taifa Gas walichokifanya Msomela ni kupanda mbegu ya Mabalozi wa kudumu ambao watakuwa na wataendelea kuwa wateja wenu daima.

"Imarisheni huduma hii hapa Msomela na jirani kuzunguka Msomela ili wananchi hawa gesiikiisha wasipate tabu mahala pa kwenda kubadilisha."

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Taifa Gas, Davis Deogratius amesema timu yake tayari imeshafanya mchakato wa kuwa na mawakala hapo Msomela tena wazawa, hivyo wasiwe na wasiwasi kwani gesi ikiwaishia wataipata Msomela na wale ambao hawajabahatika kupata mitungi ya Taifa Gas tayari ipo itakuwa inauzwa kwa bei nafuu.
Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Wakili Albart Msando amewashukuru Taifa Gas kwa msaada mkubwa kwa Wananchi wake wa Msomela na aliendelea kuwaomba kuwa wananchi wake ni wengi hapa watapata nusu yao tu na nusu bado hivyo wakipata nafasi tena wasiwasahau Wananchi wa Msomela waliokosa.











Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima, R. K akifanya mahojiano kwenye kipindi cha Jambo kinachorushwa na TBC1 jijini Dar es Salaam leo tarehe 17 Mei, 2024
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima, R. K akifafanua jambo wakati wa mahojiano kwenye kipindi cha by Jambo kinachorushwa na TBC1 jijini Dar es Salaam leo tarehe 17 Mei, 2024. Kulia ni mtangazaji wa kipindi hicho, Janeth Leornard na Rajab Rajab.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima, R. K akifafanua jambo wakati wa mahojiano kwenye kipindi cha by Jambo kinachorushwa na TBC1 jijini Dar es Salaam leo tarehe 17 Mei, 2024. Pamoja nae ni mtangazaji wa kipindi hicho, Janeth Leornard.
Mtangazaji wa kipindi Jambo Tanzania kinachorushwa na TBC1, Bi.Janeth Leornard akimuuliza swali Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima, R. K akifanya mahojiano kwenye kipindi cha by Jambo kinachorushwa na TBC1 jijini Dar es Salaam leo tarehe 17 Mei, 2024. Kushito ni Rajab Rajab mtangazaji mwenza orwa kipindi hiko.
*************
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utakuwa na mambo mapya kadhaa ikiwa ni pamoja na kuwaandikisha wafungwa kwa upande wa Tanzania Bara na wanafunzi wa vyuo vya mafunzo kwa upande wa Zanzibar na kuwaruhusu wapiga kura kuanzisha mchakato wa kuboresha taarifa zao kwa njia ya mtandao.

Akizungumza wakati wa mahojiano maalum kwenye kipindi cha Jambo kinachorushwa hewani na kituo cha televisheni cha TBC1 jijini Dar es Salaam leo tarehe 17 Mei, 2024, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima R. K amesema kuwa Tume tayari imeweka utaratibu wa kuwaandikisha wafungwa na wanafunzi hao na mfumo wa kuboresha taarifa mtandaoni upo tayari.

Kailima amefafanua kuwa utaratibu wa kuandikisha wafungwa na wanafunzi utazingatia matwaka ya sheria ambapo waliohukumiwa kifungo cha chini ya miezi sita ndio watakaoandikishwa.

Akizungumzia suala la kuanza mchakato wa uboreshaji wa Daftari mtandaoni, Bw. Kailima amesema Tume imejenga mfumo ujulikanao kama OVRS (Online Voters Registration System) utakaomwezesha mpiga kura anayeboresha taarifa zake kuanzisha mchakato mtandaoni na baadae kwenda kwenye kituo ili amalizie taratibu na kupata kadi yake ya mpiga kura.

Uboreshaji wa taarifa kwa njia ya mtandao una masharti, kwa wale ambao wanataka kurekebisha taarifa zao ni lazima wawe na namba ya NIDA, lakini, mpiga kura anayehamisha taarifa zake hatalazimika kuwa na namba ya NIDA., amesema Bw. Kailima.

Amefafanua kuwa namba ya NIDA ni muhimu kwa ajili ya kufanya uhakiki wa taarifa za mpiga kura ambazo zinarekebishwa kwenye Daftari.

Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi amefafanua kuwa, wanaokwenda vituoni kujiandikisha kwa mara ya kwanza hawatalazimika kuwa na namba ya NIDA.

Akitoa hotuba ya kutangaza tarehe ya uzinduzi wa uboreshaji wa Daftari ambao unatarajiwa kufanyika mkoani Kigoma tarehe 01 Julai, 2024, Mwemyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele alisema kuwa kwa Tanzania Bara kuna vituo vya kuandikisha wapiga kura 130 vilivyopo kwenye magareza na kwa Zanzibar kuna vituo 10 vilivyopo kwenye Vyuo vya Mafunzo.
Mhandisi. Joyce Kisamo akiwa mwenye furaha baada ya kukabidhiwa TUZO ya LUCE ya mwanamke aliyefanya vizuri katika nishati, mazingira na sekta endelevu (Legacy Women Category).
🔴Ni Tuzo ya kutambua mchango wa mwanamke aliyefanya vizuri katika nishati, mazingira na sekta endelevu
Ni tu

Na. Mwandishi wetu
Mtanzania Mha. Joyce Kisamo kutoka Wizara ya Nishati amekua muafrika wa pili kutwaa tuzo ya LUCE ya mwanamke aliyefanya vizuri katika nishati, mazingira na sekta endelevu.

Mnigeria Onyinye Anene-Nzelu ambaye ni Mkuu wa Gridi Ndogo katika Ufikiaji wa Nishati nchini Nigeria, aliwahi kunyakua Tuzo katika kundi la wanawake chipukizi 2023.

Joyce, ambaye ni Kaimu Kamishna Msaidizi wa Petroli kutoka Wizara ya Nishati alibuka mshindi wa shindano hilo la Tuzo za LUCE katika kundi la Mwanamke mwenye uzoefu na aliyeacha alama na kuwashinda wanawake wengine 15 kutoka mataifa mbalimbali ya Ulaya na Asia.

Zaidi ya kura 2,000 zilipigwa duniani kote na kura 600 zilitosha kumpa ushindi Mha. Joyce ambaye alikuwa mwafrika pekee na katika kinyang’anyiro hicho ameibuka mshindi kwa kuacha alama nyingi katika utendaji wake wa kazi (Legacy Women Category).

Kwa ushindi huo Joyce ametambulika kimataifa kuwa Mwanamke mwenye uzoefu, aliyefanyakazi na kuacha alama zenye manufaa kiuchumi, kimazingira na kijamii katika Sekta Endelevu hususani Nishati Safi na Endelevu.

Makabidhiano ya tuzo hiyo yamefanyika leo tarehe 16 Mei,2024 huko Florence nchini Italy kisha mshindi atahudhuria Mkutano wa masuala ya Nishati Safi na Endelevu. (Flagship Conference) kuanzia tarehe 23 hadi 25 Mei, 2024 katika European University Institute.

Tuzo za LUCE, zimefanyika kwa mara ya pili na linaandaliwa na mpango wa Lights on Women kwa ushirikiano na Landwärme na Edison, linalenga kutambua na kusherehekea mchango mkubwa wa wanawake.

Lengo la kuanzisha mashindano hayo ni kutetea majukumu muhimu ya wanawake kuelekea matumizi bora ya nishati endelevu.

Dar es Salaam. Nani alishawahi kufikiria kwamba itafika siku ambayo vile unavyolinda simu yako dhidi ya uhalifu wa mtandaoni ndivyo itakavyokuja kuwa sawa na kwa luninga yako?

Ndiyo, luninga yako nayo inahitaji ulinzi wa taarifa zako za siri, kama ulikuwa haufahamu au hautilii maanani basi leo utajifunza kitu.

Maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) yamepelekea mwingiliano wa vifaa tofauti vya kidigitali vinavyounganishwa na mtandao wa intaneti. Kwa mfano, sasa mtu anaweza kusimamia na kufuatilia mwenendo wa matumizi ya vifaa tofauti vya umeme nyumbani kwake kama vile luninga, mashine ya kufulia, na kiyoyozi mahali na muda wowote alipo.

Mwingiliano huu humlazimu mtumiaji wa vifaa kuweka taarifa zake za siri ili kuweza kuunganishwa navyo na hatimaye kuvisimamia kwa urahisi mahali popote alipo. Hivyo mtu hujikuta anaingiza taarifa zake binafsi kama vile majina, namba za simu, barua pepe, pamoja na nywila.

Bila shaka hii ni faida nyingine inayotokana na maendeleo ya teknolojia na mawasiliano. Lakini tunajilindaje dhidi ya hatari zinazokuja na mabadiliko haya? Watu wengi hudhani kwasababu luninga ni kifaa ambacho tunakitumia na kukiacha nyumbani au sehemu zetu kazi basi hakipo hatarini kushambuliwa na uhalifu wa mtandaoni.

Ukweli ni kwamba tunapaswa kuwa makini na uhakika wa usalama wa taarifa zetu binafsi katika vifaa vyote vya kiteknolojia na mawasiliano tunavyovitumia.

Kampuni ya Samsung kwa kuliona hilo mwaka 2013 ilitambulisha programu ya Knox kwa ajili ya kulinda mifumo ya uendeshaji na vifaa vyake vya kielekroniki.

Samsung Knox ni jukwaa la biashara la kupangilia na kudhibiti vifaa vya mkononi - ikileta ufanisi na kutoa matumizi mahususi katika sekta mbalimbali. Huifanya miundombinu ya vifaa vya mkononi ikiwa imeunganishwa, salama na yenye tija.

Tangu kuanzishwa kwake zaidi ya miaka kumi sasa, imefanikisha ulinzi wa vifaa vya Samsung takribani bilioni mbili na inatumika kusimamia vifaa zaidi ya milioni 150. Ikiwa inaaminiwa duniani kote, Knox imesaidia biashara zaidi ya 35,000 kufanikisha malengo yake kwenye mataifa tofauti.

Hivyo, ukiwa kama mtumiaji wa luninga za Samsung haupaswi tena kuwa na wasiwasi kuhusu taarifa zako binafsi ulizoziingiza ili kunufaika na huduma mbalimbali zinazotumia mtandao wa intaneti.
Samsung Knox hutambua kikamilifu matishio ya udukuzi yanavoweza kutokea kwa wakati halisi, ikiripoti mabadiliko yoyote ambayo hayajaidhinishwa. Inathibitisha kurasa tofauti za tovuti zinazofikiwa na watumiaji, ikizuia kwa hiari tovuti hatarishi ili kulinda taarifa binafsi za mtumiaji na faragha yake. Inahakikisha ulinzi thabiti wa taarifa binafsi za watumiaji kupitia muunganisho salama na Samsung Knox Vault, kichakataji mahususi kwa usalama.

Luninga za Samsung zinalindwa dhidi ya hatari za uhalifu wa mtandaoni kutokana na uwepo wa program ya Knox ambayo huifanya mifumo ya uendeshaji na kifaa kuwa salama.

Unaweza kuwa unajiuliza kwanini ni muhimu kutumia luninga inayozingatia usalama wa taarifa zako binafsi. Lakini kumbuka kwamba ujio wa luninga za kisasa umekuja na fursa ya matumizi ya huduma tofauti zilizounganishwa na intaneti kama vile majukwaa ya mpira, filamu, michezo, burudani na kuperuzi taarifa mbalimbali, ambazo kwa namna moja ama nyingine zinahitaji uingize taarifa zako binafsi.

Arusha 17 Mei 2024 - Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuendelea kutengeneza faida kubwa inayoiwezesha benki hiyo kutoa gawio kwa wanahisa wake kutokana na uwekezaji wao ndani ya benki hiyo.

Rais Mwinyi alitoa pongezi hizo wakati akifungua semina ya uwekezaji na elimu ya fedha iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wanahisa wake na Watanzania kuelekea Mkutano Mkuu wa 29 wa Wanahisa utakaofanyika Jumamosi Mei 18, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).

“Nadhani sitakuwa nimekosea nikisema ongezeko la faida baada ya kodi ambayo Benki yetu ya CRDB imepata mwaka jana kufikia Sh bilioni 424 kulinganisha na Sh bilioni 351 mwaka 2022, ni ukuaji mkubwa wa faida kupata kutokea,” alisema Rais Mwinyi.

Alisema kuwa Benki ya CRDB imeendelea kudhihirisha kivitendo kuwa “Benki kiongozi” nchini kwani kila mwaka imekuwa ikiendelea kutoa faida ya uwekezaji kwa wanahisa wake huku akizitaka taasisi nyengine za umma na binafsi kuiga mfano.

“Nimefurahishwa pia kusikia mwaka huu Bodi ya Wakurugenzi imekuja na pendekezo la ongezeko la asilimia 11 ya gawio kwa hisa. Wanahisa wa Benki ya CRDB mnastahili kutembea kifua mbele kwa ongezeko hili,” aliongezea Rais Mwinyi.
Rais Mwinyi pia aliipongeza Benki ya CRDB kwa kuandaa semina ya elimu ya fedha na uwekezaji kwa ajili ya wanahisa wake na Watanzania huku akibainisha kuwa umahiri wa masuala ya fedha wa wananchi ni moja ya msingi muhimu wa maendeleo ya watu wa taifa lolote duniani.

“Niwapongeze Benki ya CRDB kwa kuongoza katika utoaji wa elimu ya masuala ya fedha kwa Watanzania. Siku chache zilizopita, mliandaa semina mliyoiita CRDB Bank Uwekezaji Day, mimi niliifuatilia kupitia televisheni,” Rais Mwinyi alisema huku akiitaka benki hiyo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kuongeza ujumuishi wa kifedha.

Katika hotuba yake, Rais Mwinyi pia alisisitiza umuhimu wa sekta ya fedha katika maendeleo ya taifa, akitambua mchango mkubwa wa Benki ya CRDB katika kuimarisha uchumi wa Tanzania, bara na Zanzibar. Alieleza jinsi Benki ya CRDB imekuwa mshirika muhimu katika kuendeleza dhana ya Uchumi wa Buluu, kupitia programu kama vile 'INUKA na Uchumi wa Buluu', ambazo zimechangia sana katika sekta za utalii, kilimo, ufugaji, uvuvi, mafuta, biashara, na ujasiriamali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay alisema benki hiyo ikiwa benki ya kizalendo inayomilikiwa na Watanzania kwa zaidi ya asilimia 80, inajivunia kuendelea kukuza thamani ya uwekezaji wa wanahisa wake ikiwamo Serikali ambayo inamiliki asilimia 36 ya hisa katika benki hiyo.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni mwanahisa wa Benki hiyo kupitia Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Zanzibar (ZSSF). Dkt. Laay amewakaribisha Watanzania wengine kuwekeza ndani ya Benki ya CRDB ili nawao waanze kunufaika na gawio nono ambalo limekuwa likitolewa na Benki hiyo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela alisema malengo ya semina hiyo ni kuwajengea uwezo Wanahisa wao pamoja na Watanzania wengine ili kuwajengea uwajibikaji wa kifedha na kuongeza ushiriki katika fursa za uwekezaji hususan katika soko la hisa la Da es Salaam.

“Kwa kutoa elimu hii Wanahisa wetu pia wanapata kufahamu zaidi faida za kuwekeza katika Benki yao ya CRDB, hivyo basi kuongeza uwekezaji na kupata faida nono zaidi, lakini pia kuwahamasisha na Watanzania wengine pia kuwekeza katika hisa hususan za Benki ya CRDB na kuanza kupata gawio,” aliongezea Nsekela.

Aidha, Nsekela alimshukuru Rais Mwinyi kwa ushirikiano wa kimkakati na mazingira mazuri ya biashara ambayo ndio chachu ya utendaji mzuri wa benki hiyo. Kadhalika, alimhakikishia Mheshimiwa Rais kuwa Benki ya CRDB itaendelea kuwezesha uchumi wa Zanzibar kwa kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo hususan katika kuwawezesha wananchi kunufaika na fursa za Uchumi wa Buluu.

Katika semina hiyo, mada mbalimbali zilijadiliwa, ikiwa ni pamoja na Ujumuishi wa Kifedha, Uwekezaji katika Hisa, Hatifungani ya Kijani ya Benki ya CRDB, Wosia na Mirathi, pamoja na Kinga dhidi ya Majanga.

Semina ya Wanahisa iliyofanyika leo ni sehemu ya maandalizi kuelekea Mkutano Mkuu wa 29 wa Benki ya CRDB utakaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (AICC) na kupitia Mtandao. Mkutano huo unatarajiwa kuaanza saa 3 asubuhi, ambapo watu wa mtandaoni wataweza kujiunga kupitia link https://escrowagm.com/crdb/login.aspx au kupitia SimBanking App.


Benki ya CRDB imeweka muongozo wa jinsi ya kushiriki mkutano mkuu kwa njia ya mtandao kupitia tovuti yake ya www.crdbbank.co.tz, mitandao yetu ya kijamii ya Instagram, twitter, lakini pia maelekezo yametumwa kwa ujumbe mfupi kwa Wanahisa.
Sehemu ya Wanahisa wakiwa katika Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB ambayo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) kuelekea Mkutano Mkuu wa Benki hiyo utakaofanyika hapo kesho.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda akizungumza katika Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB ambayo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) kuelekea Mkutano Mkuu wa Benki hiyo utakaofanyika hapo kesho.
Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar, Saada Mkuya Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB ambayo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) kuelekea Mkutano Mkuu wa Benki hiyo utakaofanyika hapo kesho.















Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Wakili Albart Msando(kulia) akimkabidhi mtungi wa Taifa Gas Shekh wa Wilaya ya Handeni, Shaban Kizulwa wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi 300 ya Taifa Gas Bure kwa wakazi wa wilaya ya Handeni mjini.Ikiwa ni Kampeni maalumu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia Suluhu Hassan ya kumtua Mama mzigo wa kuni na kuhifandhi mazingira kwa kutumia nishati safi ya Taifa Gas.Katikati kulia ni Maneja mahusiuano wa Taifa Gas, Angela Bhoke na Maneja Mauzo wa Maduka, Nanzighe Nyambera.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Wakili Albart Msando(kulia) akimkabidhi mtungi wa Taifa Gas Kiongozi wa Wakina Mama Wajasiliamali Wilaya ya Handeni, Mwajabu Mhina wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi 300 ya Taifa Gas bure kwa wakazi wa wilaya ya Handeni mjini.Ikiwa ni Kampeni maalumu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia Suluhu Hassan ya kumtua Mama mzigo wa kuni na kuhifandhi mazingira kwa kutumia nishati safi ya Taifa Gas.Katikati kulia ni Maneja mahusiuano wa Taifa Gas, Angela Bhoke na Maneja Mauzo wa Maduka, Nanzighe Nyambera.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Wakili Albart Msando(kulia) akimkabidhi mtungi wa Taifa Gas Mama lishe, Bahati Shahiri wa Soko kuu la Handeni wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi 300ya Taifa Gas Bure kwa wakazi wa wilaya ya Handeni mjini.Ikiwa ni Kampeni maalumu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia Suluhu Hassan ya kumtua Mama mzigo wa kuni na kuhifandhi mazingira kwa kutumia nishati safi ya Taifa Gas.Katikati kulia ni Maneja mahusiuano wa Taifa Gas, Angela Bhoke na Maneja Mauzo wa Maduka, Nanzighe Nyambera.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Wakili Albart Msando(kulia) akimkabidhi mtungi wa Taifa Gas Afisa Tarafa wa kwa Msisi, Lugaila Ngwabi wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi 300 ya Taifa Gas bure kwa wakazi wa wilaya ya Handeni mjini.Ikiwa ni Kampeni maalumu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia Suluhu Hassan ya kumtua Mama mzigo wa kuni na kuhifandhi mazingira kwa kutumia nishati safi ya Taifa Gas.Katikati kulia ni Maneja mahusiuano wa Taifa Gas, Angela Bhoke na Maneja Mauzo wa Maduka, Nanzighe Nyambera.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Wakili Albart Msando(kulia) akimkabidhi mtungi wa Taifa Gas Afisa Tarafa wa Mzundu, Elizabeth Mponda wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi 300 ya Taifa Gas bure kwa wakazi wa wilaya ya Handeni mjini.Ikiwa ni Kampeni maalumu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia Suluhu Hassan ya kumtua Mama mzigo wa kuni na kuhifandhi mazingira kwa kutumia nishati safi ya Taifa Gas.Katikati kulia ni Maneja mahusiuano wa Taifa Gas, Angela Bhoke na Maneja Mauzo wa Maduka, Nanzighe Nyambera.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Wakili Albart Msando(katikati) akikata utepe kama ishaar ya uzinduzi wa Duka la Taifa Gas Wilayani Handeni wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi 300 ya Taifa Gas bure kwa wakazi wa wilaya ya Handeni mjini.Ikiwa ni Kampeni maalumu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia Suluhu Hassan ya kumtua Mama mzigo wa kuni na kuhifandhi mazingira kwa kutumia nishati safi ya Taifa Gas.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Wakili Albart Msando azungumza na baadhi ya wakazi wa Handeni mjini(hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi 300 ya Taifa Gas bure kwa wakazi wa wilaya ya Handeni mjini.Ikiwa ni Kampeni maalumu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia Suluhu Hassan ya kumtua Mama mzigo wa kuni na kuhifandhi mazingira kwa kutumia nishati safi ya Taifa Gas.
Wakazi wa Wilaya ya Handeni wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Wakili Albart Msando(hayupo pichani) ) wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi 300 ya Taifa Gas bure kwa wakazi wa wilaya ya Handeni mjini.Ikiwa ni Kampeni maalumu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia Suluhu Hassan ya kumtua Mama mzigo wa kuni na kuhifandhi mazingira kwa kutumia nishati safi ya Taifa Gas.
Meneja mahusiano wa Taifa Gas, Angela Bhoke azungumza na baadhi ya wakazi wa Handeni mjini(hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi 300 ya Taifa Gas bure kwa wakazi wa wilaya ya Handeni mjini.Ikiwa ni Kampeni maalumu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia Suluhu Hassan ya kumtua Mama mzigo wa kuni na kuhifandhi mazingira kwa kutumia nishati safi ya Taifa Gas.
Mkuu wa Wilaya akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakazi wa handeni waliopata mitungi ya Taifa Gas bure. Jumla ya mitungi 200 imegawiwa bure kwa wakazi wa handeni mjini.
Wakina Mama Lishe wa Soko Kuu la Wilaya ya Handeni Mjini wakifurahia Majiko ya Taifa Gas mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni , Wakili Albart Msando. Ikiwa ni Kampeni maalumu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia Suluhu Hassan ya kumtua Mama mzigo wa kuni na kuhifandhi mazingira kwa kutumia nishati safi ya Taifa Gas.Wakazi wa Wilaya ya Handeni Mjini wakikabidhiwa mitungi ya Taifa Ges bure kwa utaratibu maalum ulivyopangwa.