TRENDING NOW






Na Munir Shemweta, MLELE

Mkazi wa kijiji cha Luchima katika kata ya Majimoto halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi Bw. Aseni Jandikile ametoa shilingi elfu tano kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na juhudi zake za kuwaletea maendeleo wananchi.

Kiasi hicho cha pesa kimekabidhiwa kwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda tarehe 3 Mei 2024 wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Luchima alipokwenda kuzungumza nao wakati wa ziara yake ya kuwafariji wananchi waliopatwa na mafuriko katika jimbo lake la Kavuu.

‘’Nampongeza rais kwa vitendo kabisa naomba mhe, mbunge leo nikikabidhiwa fedha taslimu shilingi elfu tano umpelelekee Mhe, Rais ’’ alisema.

Kwa mujibu wa mwananchi huyo, uamuzi wake unatokana na kuwiwa na uongozi bora na utendaji kazi wa Rais Samia hasa kwa kuwajali wananchi wa Luchima ambapo mbali na mambo mengine amewajali kwa kutoa fedha milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati aliyoieleza imewakomboa wananchi wa kijiji hicho.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda amesema atahakikisha kiasi hicho cha fedha kilichotolewa na mwananchi huyo kinamfikia mhe, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Amempongeza mwananchi huyo wa kijiji cha Luchima wa uamuzi wake wa kutoa kiasi hicho cha fedha kama ishara ya kukubali juhudi na kazi kubwa inayofanywa na Mhe, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Luchima na Tanzania kwa ujumla.

Amewaaleleza wananchi wa kijiji hicho kuwa, Rais Samia anawapenda sana na amekuwa akisaidia juhudi mbalimbali za maendeleo kwenye jimbo la Kavuu na kutaja baadhi ya juhudi hizo kuwa ni pamoja na kutoa fedha za ujenzi wa hospitali, shule, barabara pamoja na upatikanaji wa huduma za maji.Mhe, Pinda amefanya ziara katika jimbo lake la Kavuu kuwafariji wananchi waliopatwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa na kuathiri miundiombinu ikiwemo madaraja.Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda akimpongeza mkazi wa kijiji cha Luchima katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi Bw. Aseni Jandikile aliyetoa shilingi elfu tano kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na juhudi zake za kuwaletea maendeleo wananchi tarehe 2 Mei 2024.Mkazi wa kijiji cha Luchima katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi Bw. Aseni Jandikile akizungumza mara baada ya kumkabidhi shilingi elfu tano Naibu Waziri wa Ardhi na Mbunge wa jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda aliyoitoa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na juhudi zake za kuwaletea maendeleo wananchi tarehe 3 Mei 2024.Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa jimbo la Kavuu Mhe. Geophrey Pinda akimpongeza mkazi wa kijiji cha Luchima katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi Bw. Aseni Jandikile aliyetoa shilingi elfu tano kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na juhudi zake za kuwaletea maendeleo wananchi tarehe 2 Mei 2024.
Na Munir Shemweta, MLELE

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kauu Mhe, Geophrey Pinda ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kujenga mahusiano mazuri na wafanyabiashara wa eneo Majimoto katika halmasauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi.

Mhe, Pinda ametoa kauli hiyo tarehe 3 Mei 2024 wakati wa kikao cha pamoja kati ya Maafisa wa TRA Makao makuu na wafanyabiashara wa eneo la Majimoto kilichofanyika katika halmashauri ya Mpimbwe.

Kikao hicho cha siku moja kinafuatia kuwepo malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara kuwa wamekuwa wakinyanyaswa na maafisa wa TRA katika eneo hilo jambo walilolieleza kuwa limekuwa likisababisha usumbufu katika biashara zao.

‘’Mimi kama mbunge wa jimbo la Kavuu niko tayari kutoa ushirikiano na TRA lakini ushirikiano huo uende sambamba na mamlaka hiyo kujenga mahusiano mazuri na wafanyabiashara ‘’ amesema Mhe, Pinda

Amesema, ni wajibu wake kuhakikisha maisha ya wafanyabiashara katika eneo la Majimoto yanakuwa rafiki na kusisitiza kuwa, eneo hilo linapoteza wateja wengi na sababu kuwa na mahusiano mabovu na walipa kodi.

Aidha, Mhe, Pinda amewataka maafisa wa TRA katika eneo hilo kutokuwa na dharau kwa wafanyabiashara na kuhoji unapomdharau mlipa kodi unategemea kitu gani huku akisisitiza mamlaka hiyo kutoa huduma nzuri kwa kwa wateja.

Kwa mujibu wa Mbunge huyo wa jimbo la Kavuu, Mamlaka ya Mapato Tanzania lazima maafisa wake wawe rafiki na wafanyabiashara ili kuondoa vikwazo vinavyoweza kupeleka mkwamo kwa wafanyabiashara.

Amebainisha kuwa, TRA pamoja na mambo mengine lazima ijikite kutoa elimu kwa mlipa kodi kama ambavyo maafisa wake walivyofanya kwa kwenda kwa wafanyabiashara wa Majimoto huku akiwataka maafisa hao kuacha kabisa siasa katika shughuli za kibiashara. ‘’Nasema haya ili mje na mageuzi makubwa kwa lengo la kuboresha’’. Amesema Mhe, Pinda

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Mpimbwe Bi. Shamim Daud amesema, zaidi ya asilimia hamsini ya mzunguko wa fedha katika halmashauri yake inatoka eneo la Majimoto na ndiyo maana halmashauri yake imeweka uwekezaji mkubwa katika eneo hilo ili kuhakikisha huduma za jamii zinaimarishwa na kupunguza changamoto kwa watu wanaoingia na kutoka eneo hilo.

‘’Kwa hiyo tunashukuru na tunatumaini kikao hiki watu watakapotoka watakuwa wamejifunza na TRA watakuwa wameelewa changamoto za maeneo hayo na kuwaletea mabadiliko makubwa’’. Amesema Mhe, Pinda.
Mbunge wa jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe, Geophrey Pinda akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu na Wafanyabiashara wa eneo la Majimoto katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi tarehe 3 Mei 2024.Mkuu wa Wilaya ya Mlele Alhaji Majid Mwanga akizungumza wakati wa kikao cha Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu na Wafanyabiashara wa eneo la Majimoto katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi tarehe 3 Mei 2024. Kushoto ni Naibu Waziri wa Ardhi na Mbunge wa jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey PindaMkurugenzi wa Halmashauri ya Mpimbwe Bi. Shamim Daud akizungumza katika kikao Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wafanyabiashara wa eneo la Majimoto katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi tarehe 3 Mei 2024.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe, Geophrey Pinda akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wafanyabiashara wa eneo la Majimoto katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi tarehe 3 Mei 2024. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mlele Alhaji Majid Mwanga na kushoto ni Mkurugenzi wa halmashauri ya Mpimbwe Bi. Shamim Daud.



Sehemu ya washiriki wa kikao baina ya Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wafanyabiashara wa eneo la Majimoto katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi tarehe 3 Mei 2024

 


Na Munir Shemweta, MLELE

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu katika halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi Mhe, Geophrey Pinda amekabidhi baiskeli za walemavu wa miguu ikiwa ni jitihada za kuwasaidia watu wenye ulemau.

Mhe, Pinda amekabidhi baiskali tarehe 2 Mei 2024 wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Kirida katika Kata ya Mamba halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele mkoa wa Katavi.

Baiskeli iliyokabidhiwa kwa mlemavu Bi. Adela John mkazi wa Kirida ni sehemu ya baiskeli nne zilizotolewa kwa walemavu wa miguu wa jimbo la Kavuu ikiwa ni njia ya kuwasaidia usafiri wa kuwawezesha kwenda maeneo mbalimbali.

Akizungumza wakati wa kukabidhi baiskeli hiyo, Mbunge wa jimbo hilo na Naibu Waziri wa Ardhi Mhe, Pinda amesema kuwa, anatambua adha wanayoipata walemavu wa miguu katika jimbo lake ndiyo maana ameona ipo haja ya kuwapatia baiskeli zitakazowasaidia kwenda katika shughuli zao.

‘’Ni matumaini yangu kuwa baiskeli hii itakuondolea adha uliyokuwa ukiipata na kwa sasa itakusaidia sana wakati wa kwenda katika shughuli zao mbalimbali’’ alisema Mhe, Pinda.

Mapema kwenye mkutano wake na wananchi wa kijiji cha Kirida katika kata ya Mamba halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele mkoa wa Katavi, Mhe, Pinda aliwaeleza wananchi wa kijiji hicho kuwa, pamoja na kukabiliwa na majukumu ya uwaziri lakini amekuwa akifanya juhudi ya kuwatumikia katika kuwaletea maendeleo.

Amezitaja juhudi hizo kuwa ni pamoja na ujenzi wa barabara, zahanati na vituo vya afya, madaraja na shule za msingi na sekondari sambamba na upatikanaji huduma za umeme na maji.

‘’Pamoja na kwamba hamnioni mara kwa mara nikija hapa Kirida kutokana na majukumu niliyo nayo lakini nimekuwa nikifanya kazi kubwa ya kuwaletea maendeleo na haya maendeleo mnayo yaona kama vile ujenzi wa bararbara, shule, zahanati na vituo vya afya, zote ni jitihada ambazo ninazifanya’’. Alisema Mhe, Pinda.

Awali wananchi wa Kijiji cha Kirida katika kata ya Mamba walimueleza mbunge wa jimbo hilo kuwa wanakabiliwa na changamoto malimbali ikiwemo kutofanyika vikao vya kijiji kwa ajili ya kujua mapato na matumizi, kuwekewa alama za mipaka maeneo ya nyumba zao kwa madai kuwa makazi hayo yapo kwenye kingo ya mto na hivyo kutakiwa kuhama wakati mto ndiyo umehama.Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu katika halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi Mhe, Geophrey Pinda (Kushoto) akimkabidhi Baiskeli Mlemavu wa Miguu Bi. Adela John wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Kidira katika kata ya Mamba halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi Mei 2, 2024. Katikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpimbwe Silas Ilumba.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu katika halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi Mhe, Geophrey Pinda na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpimbwe Silas Ilumba wakimuangalia Bi. Adela John ambaye ni mlemavu wa miguu mara baada ya kumkabidhi baiskeli tarehe 2 Mei 2024. 
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kirida katika kata ya Mamba halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi wakati wa ziara yake katika jimbo la Kavuu Mei 2, 2024.
Beda Andrea mkazi wa kijiji cha Kirida Kona akiwasilisha changamoto zake kwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Kirida kata ya Mamba halmashauri ya Mpimbwe Mei 2, 2024.


Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kirida katika kata ya Mamba halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda (Hayupo pichani) wakati wa mkutano wa hadahara uliofanyika kijiji cha Kirida Mei 2, 2024. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian akikagua gwaride kabla ya kufunga mafunzo ya awali ya ya Kijeshi kwa vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT kikosi cha Jeshi 838 Maramba.
MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian akikagua gwaride kabla ya kufunga mafunzo ya awali ya ya Kijeshi kwa vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT kikosi cha Jeshi 838 Maramba.
MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian akizungumza wakati alipofunga mafunzo ya awali ya ya Kijeshi kwa vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT kikosi cha Jeshi 838 Maramba.
Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi la Ulinzi Tanzania Brigedia Jenerali Abubakari Charo akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo ya awali ya ya Kijeshi kwa vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT kikosi cha Jeshi 838 Maramba.
Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Kanali Elias Sikaponda akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo ya awali ya ya Kijeshi kwa vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT kikosi cha Jeshi 838 Maramba.
MKUU wa Kikosi cha Jeshi 838 JKT Maramba Kanali Ashraf Hassan akizungumza wakati wa mafunzo hayo.

Na Oscar Assenga, MKINGA.

MKUU wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob Mkunda amesema mafunzo ya awali ya ya Kijeshi kwa vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT kikosi cha Jeshi 838 Maramba huku akieleza umuhimu wa vijana hao ni mkubwa kutokana na kwamba wanaingia kwenye Jeshi la akiba ambalo inapotokea hitajiko la ulinzi wa Taifa wanaitwa kwa mujibu wa sheria.

Jenerali Mkunda aliyasema hayo Jumanne Aprili 30 mwaka huu wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo ambapo aliwakilishwa na Brigedia Jenerali Abubakari Charo ambapo alisema kutokana na miongozo mbalimbali iliyopo kwa mafunzo hayo ya vijana hasa kwa kuzingatia kwamba vijana hao wanapohitimu mafunzo yao wanaingia kwenye jeshi la akiba.

Alisema kwamba linapotokea hitajiko la ulinzi wa Taifa na Rais na Amri Jeshi Mkuu akatangaza hali ya hatari vijana hao wanaitwa kwa mujibu wa sheria kwenda kuungana na Jeshi la Wananchi (JWTZ) kulinda ulinzi wa Taifa.

Aidha alisema kutokana na umuhimu wa vijana kwenye Jeshi hilo wanapenda kuona wanafikia viwango na malengo ya mafunzo hayo na amewaona wamefikia viwango vinavyotakiwa huku akieleza yanawajenga kwenye nidhamu, ukakamavu, uzalengo, uhodari wa kujiamini na kulipenda taifa lao.

“Nichukue fursa hii kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi kutoa shukrani kwa dhati kwa Serikali kwa juhudi zinazofanyika kuhakikisha mazingira ya mafunzo kwa vijana ndani ya JKT yanaboreshwa”Alisema

“Kwani katika mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali imetoa kiasi cha sh Milioni 950 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni kwa vijana wanaojiunga na JKT fedha hizo zimeweza kujenga mabweni 12 kila moja lenye uwezo wa kuchukua vijana 120 hivyo kusaidia kikosi kuongeza uwezo kuchukua vijana 1440 na hii ni ishara za wazi kwamba serikali inatambua na kuthamini mafunzo ya vijana wa JKT”Alisema

“Lakini pia ujenzi wa vyoo vitano ambapo kila choo kina matundu 22 vitatumika kwa vijana hilo sio suala dogo ni jambo kubwa ambalo serikali imefanya kwa mazingira hayo wanawaomba vijana ambao hawapati fursa kujiunga na JKT wasije kufikiria wametengwa na kunyimwa fursa bali lengo vijana wote wapite Jkt na wale vijana wanaomaliza kidato cha sita”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba Jeshi la Kujenga Taifa litakuwa likiendelea kuongozewa uwezo huku akieleza wanathamini juhudi za serikali katika kuboresha mazingira ya jeshi hilo ambapo mafunzo ambayo wameyapata yatawawezesha kuajiriwa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama,sekta mbalimbali za serikali au makampuni mbalimbali .

Awali akizungumza wakati akifunga mafunzo hayo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian alisema mafunzo hayo kwa vijana wa JKT ni muhimu sana kwa vijana kwa maana wao ndio tegemeo la Taifa.

Balozi Batilda alisema Rais Dkt Samia Suluhu kupitia falsafa yake ya 4R ameendelea kusimamia na ndio maana juzi chadema walikuwa na maandamano yao wakasimamiwa vizuri na jeshi la Polisi wakafanya mkutano wao wakatembea.

Alisema kwa hakika wakawa na matumaini watapata mambo ya msingi yatakayowasaidia kujenga nchi lakini wakasikia mambo tofauti kwanini wakuu wa mikoa hawapigiri kura, kama madiwani sasa akasema hata RC akipigiwa kura atachaguliwa Tanga na RC ni msaidizi wa Rais anaweza kuhamishwa kila eneo.

“Tulitegemea kwamba hivi sasa nchi ipo kwenye kipindi kigumu na mvua zinanyesha madhara maeneo mengi barabara nyingi zimepata changamoto na maeneo mengi lami zimepasuka changamoto ni nyingi vita vya israel vinaendelea duniani gharama zinapanda bei ya dola ipo kubwa kulingana na bei yetu sisi tukaona haja hoja zao za za kwamba hazikuwasaidia wakapata mawazo mbadala hazipo"Alisema.

Hata hivyo Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Kanali Elias Sikaponda alisema kwamba alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa sababu yanaleta tija kwa vijana katika shughuli za kujitegemea huku akiwataka kujiepusha na matumizi ya dawa za kulevya.

Aliwataka pia vijana hao kutumia elimu waliyoipata wakaweze kutatua changamoto mbalimbali pasipo kuvunja sheria na taratibu zilizowekwa hapa nchini huku akisiistiza watumie nidhamu pekee kama silaha kwenye jambo lolote mbeleni.


Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza kuwa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kwahani lililopo Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar utafanyika tarehe 08 Juni, 2024.

Taarifa kwa umma iliyotolewa na kusainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa INEC, Bw. Kailima, R. K jijini Dodoma leo tarehe 02 Mei, 2024 imesema kwamba fomu za uteuzi kwa ajili ya uchaguzi huo mdogo zitatolewa kuanzia tarehe 17 hadi 23 Mei, 2024.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa uteuzi wa wagombea utafanyika tarehe 23 Mei, 2024 na kampeni kwa ajili ya uchaguzi huo zitafanyika kuanzia tarehe 24 Mei, 2024 hadi tarehe 07 Juni, 2024.

Tume imetangaza uchaguzi huo mdogo kufuatia taarifa ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iliyomtaarifu Mwenyekiti wa Tume kuhusu uwepo wa nafasi wazi ya ubunge katika Jimbo la Kwahani.

Spika ametoa taarifa hiyo kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 49(2) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka, 2024.

“Kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 49(1)(b) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, Tume inatoa taarifa kwa umma kuhusu uwepo wa uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Kwahani lililopo Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Tume imevikumbusha vyama vya siasa, wagombea na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia Katiba, sheria, kanuni, maadili ya uchaguzi, taratibu, miongozo na maelekezo ya Tume katika kipindi cha uchaguzi huo mdogo.

Dar es Salaam. Maeneo tofauti nchini Tanzania yanashuhudia mvua kubwa ambazo sio tu zinaathiri miundombinu na kuhatarisha usalama wa maisha ya watu bali pia inaweza kuwa hata kwa vifaa vya umeme nyumbani.

Watu wengi huingia hasara wakati vyombo vyao vya umeme walivyovinunua kwa gharama kubwa kuharibika kutokana na hitilafu za umeme. Mara nyingi matukio ya aina haya yanaweza kuzuilika endapo tahadhari zikichukuliwa mapema.

Akizungumzia kuhusu mambo muhimu ya kuzingatia, Meneja wa Bidhaa za Kieletroniki wa Samsung Tanzania, Bw. Evans Songa ametolea ufafanuzi maswali ya msingi ambayo wateja wengi wamekuwa nayo hususani kwa wanaoishi na familia au wenyewe, ili kuhakikisha usalama wa vyombo vya umeme nyumbani.

Swali: Kuna hatari zipi za kushika vyombo vya umeme kwa mikono ikiwa na maji?

Jibu: Bila shaka wote tunafahamu kwamba maji na umeme haviendani. Madhara ya kutumia vyombo vya umeme mikono ikiwa imelowana ni pamoja na mtumiaji kupigwa shoti ya umeme. Pia, unaweza kusababisha shoti kwenye kifaa chako. Kuna baadhi ya vifaa vinakuelekeza uhakikishe kuwa ni vikavu kabla ya kuchomeka katika soketi ya umeme.

Swali: Nini kinashauriwa baada ya kumaliza matumizi ya vyombo vya umeme nyumbani?

Jibu: Kuna baadhi ya watu wana kawaida ya kuacha vyombo vyao katika soketi za umeme baada ya kumaliza matumizi. Mbaya zaidi wengine husahau hata kuzima kabisa kutokana na vifaa vingi vya siku hizi ni automatic hivyo kujizima vyenyewe mara tu vikimaliza kazi iliyokusudiwa. Tabia hii inaongeza hatari ya chombo kuharibika au kuungua endapo kutatokea shoti ya umeme. Umeme kujizima na kujiwasha hususani kipindi hiki cha mvua ni kawaida hivyo unashauriwa ni vema kuzima na kuchomoa chombo chako katika soketi ya umeme baada ya kumaliza matumizi. Hii itakulinda hata endapo utatoka nyumbani kwako kwa dharura au kuendelea shughuli zingine.


Swali: Kuna faida gani ya kusafisha vyombo vya umeme mara kwa mara baada ya kumaliza matumizi?

Jibu: Inashauriwa kusafisha vyombo vyako vya umeme mara tu baada ya kumaliza matumizi. Hii itakusaidia kulinda vyombo vyako hususani kwa kuvieupusha na mazingira ambayo yanaweza kuleta kutu. Ukiachana na kusafisha pia hakikisha unakuwa unavitumia vyombo vyako mara kwa mara ili kujua kama vinafanya kazi kwa ufasaha au la. Sidhani kama utafurahi siku ambayo una uhitaji zaidi wa chombo chako na kugundua kuwa hakifanyi kazi aidha kutokana na kutokitunza au kujaribu kama kinafanya kazi mara kwa mara.

Swali: Kuna umuhimu gani wa kuwa na warantii kwa vyombo vya umeme?

Jibu: Kwanza kabisa, kwa wasiofahamu warantii ni dhamana ya muda maalumu inayotolewa kwa ajili ya matazamio ya bidhaa ili kumhakikishia mtumiaji juu ya ubora na ufanyaji kazi wa bidhaa husika. Sio kampuni zote zinatoa warantii kwa bidhaa wanazouza kwa wateja wake. Lakini kuna makampuni ambayo yanazingatia hili ili kuwaridhisha na kuwapatia amani wateja wake dhidi ya hofu ya vyombo vyao pindi vikipata hitilafu. Kwa mfano, Samsung hutoa warantii kwa bidhaa zake kwa muda wa miaka miwili na miaka 20 kwa bidhaa zenye kompresa na mota. Bidhaa hizo ni pamoja na runinga, majokofu au friji, mashine za kufulia, kupashia chakula, kiyoyozi, nakadhalika.

Ukiachana na warantii, pia humhakikishia mteja kupata huduma kutoka kwa wataalamu wao wenye weledi, huduma kwa mteja ya uhakika, vifaa halisi marekebisho yakihitajika, pamoja na kupokea taarifa za mara kwa mara kuhusu kifaa husika. Kigezo muhimu cha kupata warantii ni kununua bidhaa kutoka kwa mawakala wa bidhaa waliohakikiwa pamoja na kuwa na kadi ya warantii kwa bidhaa za nyumbani.

Kwa kumalizia, familia nyingi zinatumia vyombo vya umeme nyumbani kutokana na maendeleo ya kiuchumi yanayochochewa na uvumbuzi katika sekta ya sayansi na kiteknolojia. Kuongezeka kwa makampuni ya utengenezaji na usambazaji wa vifaa hivyo pia kumepelekea urahisi na unafuu wa upatikanaji wake. Bila kusahau kuongezeka kwa matumizi ya umeme nchini kote ambayo yanahamasisha watu kubadilika kuendana na wakati. Hivyo, ni muhimu kuchukua hatua kila mara unapokuwa haupo nyumbani kwa usalama wa vyombo vyako, wewe mwenyewe na uwapendao.